Watoto wa mjini wanasema kala mkono.
Ndicho kilichomtokea Costa Rica mara baada ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania, timu iliyojaliwa wachezaji wenye vipaji.
Usiku wa leo timu ya taifa ya Hispania imeigaragaza timu ya Costa Rica kwa kipigo cha mabao 5-0.
Alianza mlinzi wa kushoto wa Hispania anayeichezea Barcelona, Jordi Alba ambaye alipokea mpira kutoka kwa kiungo anayeichezea Manchester city, David Silva.
Akafata mshambuliaji hodari anayeichezea Chelsea, Alvaro Morata akaifungia Hispania goli la pili kabla ya David Silva kufunga mara mbili na kisha kumalizia Andres Iniesta aliyekamilisha jumla ya idadi kuwa Hispania 5-0 Costa Rica.
Post a Comment
Post a Comment