Mara baada ya jana timu ya taifa ya Sweden kumpokonya tiketi mbabe Italia katika kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Urusi, sasa Denmark naye kafanya mapinduzi.

Wananchi na raia wa Denmark watakuwa wenye kujawa na furaha, mara baada ya timu yao kufuzu kucheza michuano hiyo kwa kishindo.

Magoli 5-1 ndiyo yameipaisha Denmark dhidi ya Jamhuri ya Ireland, tena ushindi mkubwa kama huo ugenini ni sababu inayoongeza thamani na utamu wa timu hiyo katika kufuzu uko.

Magoli matatu ya Christian Eriksen ambaye anaichezea klabu ya Tottenham, goli moja la beki kisiki wa Chelsea, Andreas Christensen na jengine Ireland wakijifunga.

Hongereni Denmark.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.