Kocha wa Chelsea, Antonio Conte leo amefanya mkutano na waandishi wa habari katika kuelekea wiki nyengine ya michezo ya ligi kuu Uingereza.
Antonio Conte alipoulizwa kuhusu uwepo wa David Luiz katika kikosi cha timu hiyo mara baada ya mchezo uliopita kuwekwa nje katika mchezo dhidi ya Man utd, "kuwekwa kwa Luiz nje ni mbinu za kiunamichezo, na sio kwamba kuna uhusiano mbaya kati yangu nayeye (Luiz)." alisema kocha Antonio Conte.
"nafikiri nimefika hapa kuulizwa kuhusu timu kujiandaa vipi na mchezo ujao, sizani kama natakiwa kujibu maswali ya kuhusu mtu mmoja" aliongezea Conte kuonyesha hataki kuhojiwa sana kuhusu David Luiz.
Post a Comment
Post a Comment