Nchini Italia kwa sasa ni kama imepooza, kila mwananchi mzalendo ni kama ana huzuni, na huenda kusifanyike chochote nchini humo na hata vikifanyika basi wananchi watakuwa hawana ile hali ya kila siku. Ni kama huzuni waliyopata wananchi wa Brazil baada ya kushuhudia timu yao ikigaragazwa magoli 7-1 na Ujerumani tena ikiwa nchini kwao katika ardhi yao, ile huzuni inaweza ikawaingia wananchi wa nchi nzima ya Italia.
Mara baada ya timu yao kushindwa kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 huko nchini Urusi. Tena imeshindwa kufuzu dhidi ya timu ambayo haikutegemewa, Sweden, wakicheza bila mshambuliaji wao, mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo, Zlatan Ibrahimovic.
Alafu inapouma zaidi unashindwa kufuzu kwa tofauti ya goli 1 tu, yaani goli lile walilofungwa nchini Sweden ndilo limeifanya Italia ilie, ndilo limemfanya kipa nguli, Gigi Buffon kustaafu soka la kimataifa kwa machozi.
Kipa Gianluigi 'Gigi' Buffon alikuwa anakaribia kuweka rekodi ya mchezaji wa Italia wa kwanza kushiriki michuano sita ya kombe la dunia mfululizo, lakini goli moja la Sweden limefuta rekodi hiyo.
De Rossi, mkongwe wa klabu ya AS Roma naye ametanduka daruga kuichezea timu hiyo ya taifa akifuatiwa na Barzagli wa klabu ya Juventus, wote hao watangaza kustaafu kutokana na goli moja tu la Sweden.

Lakini kutokana na vilio vyote hivyo, na watu kuamua kutandika madaruga lakini kocha aliyeshuhudia timu yake ya Italia ikitoa machozi kama ivyo, bado ana moyo wa jiwe, Filipe Scolari alipowaliza wabrazil pale nchini kwao baada ya kipigo kizito alitangaza kuachana na timu hiyo lakini kocha wa Italia amesema bado anaendelea labda taifa limfukuze.
Chukua hii mara ya mwisho kwa Italia kutokufuzu kombe la dunia ilikuwa mwaka 1958 ambapo wakati huo kocha wa sasa Gian Piero Ventura alikuwa na miaka 9. Kwa sasa anamiaka 69 ambapo ni miaka 60 toka Italia ishindwe kufuzu.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.