Kocha wa timu ya taifa ya Wales, Warren Gatlands amempa ushauri nyota wa timu hiyo Gareth Bale ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid.
"Muhimu awe ana furaha pale alipo (Real Madrid) na kama hana furaha basi haina haja ya kuendelea kubaki" alisema kocha huyo wa Wales.
Bale hajaichezea Madrid michezo 40 kati ya 60 iliyopita akisumbuliwa na majeruhi yanayomweka nje muda mrefu.
Bale anatajwa kuweka sokoni na klabu yake ambapo Madrid inataka kiasi cha paundi milioni 85 ili kumuachia nyota huyo.
Post a Comment
Post a Comment