Ivanka Trump amejiunga rasmi na serikali ya babake ambapo atahudumu kama mfanyakazi asiyelipwa, kwa mujibu wa ikulu ya White House.
Cheo chake halisi kitakuwa Msaidizi wa Rais.
Binti huyo wa rais wa Marekani amekubali shinikizo baada ya wataalamu kuhusu maadili kukosoa mpango wake wa awali wa kutaka kuhudumu katika wadhifa usio rasmi.
Bi Trump, 35, amesema amesikia "maswali ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza kuhusu hatua yangu kumshauri rais katika nafasi yangu kama mtu binafsi".
Mumewe, Jared Kushner, ni mshauri mwandamizi wa Rais Donald Trump.
Kupitia taarifa, White House imesema ina furaha kwamba "Ivanka Trump amechukua hatua hii isiyotarajiwa katika nafasi yake kama binti wa rais".Bi Trump alisema kupitia taarifa yake kwamba amekuwa akifanya kazi "kwa nia jema na kundi la washauri wa rais White House pamoja na mshauri wake binafsi kujadili kuhusu jukumu lake"
Post a Comment
Post a Comment