Mawasiliano kati ya haiti ya kusini na makao makuu yamepotea baada ya daraja linalowatenganisha kna makao makuu Port-au-Prince, kuvunjika kutokana na mvua nzito inayoendelea kunyesha.
Kwa sasa mvua inanyesha kwa wingi magharibi mwa nchi na barabara kuu, hasa katika mji mkuu wa Port-au-Prince na Léogâne, imeanza kukumbwa na mafuriko.
Katika mji mkuu, watu wamekua na wasiwasi kuhusu mto Grise. Mto huo umekua ukisababisha upepo mkali na maafisa wa Idara za dharura wameshindwa kuwakinaisha wakazi wa mji huo. Watu wengi wamekua wakijielekeza kwenye mto huo ili kushuhudia hali hiyo ya kutisha, huku wengine wakicheka wanaposukumwa na upepo mkali unaosababidshwa na mawimbi ya mto huo. Na wale ambao wanaishi katika nyumba hatari bado wanasita kuondoka katika maeneo hayo.
Mkoa unaoathirika zaidi nchini Haiti ni Grand Sud, hasa karibu na maeneo ya Jeremie na Les Cayes. Kiwango cha mafuriko na uharibifu ni kikubwa, lakini kwa sasa, ni vigumu kujua hali halisi katika eneo lote la kusini mwa nchi.
Bado mpaka sasa haijafahamika kiwango cha uharibifu wa kimbunga hicho nchini Haiti, lakini nyumba nyingi zimebomolewa, huku barabara zikiwa hazipitiki kutokana na miti iliyoanguka pamoja na mafuriko.
Kimbunga Matthew kinatarajiwa kupiga nchini Cuba katika masaa machache kabla ya kkuelekea katika jimbo la Florida. Katika jimbo la Florida ambapo mkutano wa hadhara wa Hillary Clinton ulifutwa kwa sababu ya hatari ya kimbuga hiki.
Post a Comment
Post a Comment