Kati ya madiwani 14 wa halmashauri ya mji wa Tunduma,ni diwani mmoja pekee France Sikanyika wa Chama Cha Mapinduzi kutoka kata ya Chiwezi ndiye aliyejitokeza huku wenzie kumi na tatu wa Chadema wakiingia mitini.
Wakati viongozi hao wakionesha hali hiyo, mambo yalikuwa tofauti kwa wananchi kwani kila kona ambayo Mwenge ulipita waliushangilia kwa wingi na kwa shangwe.
Alipohojiwa na waandishi wa habari juu ya kutoshiriki kwa madiwani wa Chadema, mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Tunduma bwana Erick Mapunda amesema hajui sababu, bali kama ilivyokuwa kwa mwenzao wa CCM nao walishirikishwa kwa kupewa taarifa.
Mapunda amesema anaweza kuzungumzia kitendo hicho baadaye iwapo madiwani hao watawasilisha kwake taarifa ya sababu iliyowafanya wasishiriki mbio za Mwenge kwenye halmashauri yao.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wetu katika eneo la Mkesha wa Mwenge,walilaani kitendo kilichofanywa na madiwani wao wakisema kinaonesha kukosekana kwa uzalendo wa kudumisha na kuimarisha tunu za Taifa...
Post a Comment
Post a Comment