Wagombea urais nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wamepambana vikali katika mdahalo wa kwanza wa televisheni ambapo wamepingana katika masuala mbali mbali ikiwemo masuala ya sera, kodi, ajira na uchumi.

Kadhalika wamejibizana kuhusu Vita vya Iraq na juhudi za kukabiliana na kundi linalojiita Islamic State.
Msimamizi wa mdahalo huo Lester Holt amemwuliza mgombea wa chama cha Republican Donald Trump mbona kufikia sasa bado hajaweza wazi taarifa zake za ulipaji kodi.

Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amemshutumu mpinzani huyo wake akisema amekuwa akikwepa kulipa kodi na kudokeza kwamba hilo lina maana kwamba hakuwezi kuwa na wanajeshi, pesa za kulipa wanajeshi waliostaafu pamoja na kufadhili elimu na huduma ya afya.
Lakini tajiri huyo kutoka New York amejibu kwa kusema kwamba atatoa hadharani taarifa hizo iwapo Bi Clinton naye atakubali kutoa barua pepe 33,000 ambazo zilifutwa kutoka kwa sava yake wakati wa uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba alitumia barua pepe ya kibinafsi kwa kazi rasmi alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Bi Clinton amekubali lawama kuhusu kosa hilo na kusema hakuwezi kuwa na "kisingizio".

Kadhalika, Bw Trump amemlaumu mpinzani huyo wake kuhusu kupotea kwa ajira akisema nafasi za kazi "zinaikimbia nchi" na akalaumu mikataba duni ya kibiashara.
Amesema Bi Clinton amekuwa mtu wa "maneno mengi, bila vitendo".
Bi Clinton ameahidi kuongeza uwekezaji na kuahidi kuunda nafasi takriban 10 milioni za kazi.
Mdahalo huo ulioandaliwa jijini New York huenda ukawa mdahala uliotazamwa na watu wengi zaidi katika historia ambapo watu 100 milioni inakadiriwa walitazama mdahalo huo.

Kura za maoni zinaonyesha wawili hao wanakaribiana sana katika uungwaji mkono.
Mambo mengine makuu yaliyoibuka kwenye madahalo:
"Umekuwa ukikabiliana na ISIS maisha yako yote,'' Bw Trump amemkejeli Bi Clinton
Amesema Bi Clinton hana uwezo wa kikudhibiti ukali wa kumuwezesha kuwa rais.
Wamarekani Weusi wanaishi "katika jehanamu" nchini Marekani, Trump amesema, kwa sababu maisha yao yamekuwa hatari sana.
Akijibu kupigwa risasi kwa watu weusi, bw Trump amesema suluhu ni kurejesha utawala wa sheria.
Bi Clinton amesema akichaguliwa kuwa rais atatekeleza mageuzi katika mfumo wa sheria kwa sababu "suala la asili limekuwa likiamua mengi".

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.