Kiongozi mkuu wa kundi la Boko Haram ambalo ni kundi lenye itikadi kali la kiislamu nchini Nigeria, Abubakar Shekau ambaye mwanzoni iliripotiwa alikufa mwezi mmoja uliopita ametuma video akielezea habari hizo zilizoonea ni uzushi tu na kwamba yeye hakufa na ni mzima wa afya. Na zile ripoti na picha zote zilizotolewa zikimuonyesha kwamba yeye ni marehemu ni uongo mtupu, yeye ni mzima na hana tatizo lolote kiafya.
Na pia ilikuwa inasemekana kwamba amechaguliwa mtu mwengine kumrithi madai hayo ameyatengua na kusema yeye ni kiongozi na itabaki kuwa hivyo.
Post a Comment
Post a Comment