"Hahaaaaa!! Bado Leicester city kwenye ligi"
"Namtamani sana nimkung'ute tena meno yangu yashaota, nlikuwa kibogoyo kwa muda"
Ni tambo na maneno ambayo mashabiki na wapenzi wa Man utd wanaendelea kujitamba baada ya usiku wa jana kumbamiza kipigo cha bao 3-1 timu ya Northampton. Alianza Michael Carrick kwa bao lake swafi kabisa katika kipindi cha kwanza huku Revell wa Northampton akachomoa bao hilo kwa mkwaju wa penalt na mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Man utd walitoshana nguvu ya bao moja kwa moja na timu hiyo. Katika kipindi cha pili Ander Herrera alipiga shuti kali na kuisaidia timu yake kuwa mbele kwa mabao 2-1 kabla ya kinda wao aliye kwenye ubora akiongeza utamu wa ushindi kwa kupiga bao la 3 na mechi kuisha ubao ukisomeka Northampton 1-3 Manchester united.

Matokeo mengine ni:
Fulham 1-2 Bristol City
QPR 1-2 Sunderland
Southampton 2-0 Crystal Palace
Swansea 1-2 Manchester city
West Ham united 1-0 Accrington
Stoke city 1-2 Hull city
Tottenham 5-0 Gillingham

Huku katika ligi ya Hispania ligi yao pia imezidi kukomaa kuwa ngumu baada ya jana katika mechi ya mapema Real Madrid akitoshana nguvu na Villareal ya bao 1-1, huku katika dimba la Camp nou wenyeji Barcelona pia wakitoka sare ya bao 1-1 na Atletico Madrid, goli la Barcelona likifungwa na Ivan Rakitic akipokea pasi murua kutoka kwa Andres Iniesta huku goli la Atletico akitupia kinda wao mwenye kiwango kitamu Correa.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.