Baada ya kuchezwa kwa kombe la EFL pale Uingereza kwa siku mbili mfululizo, siku ya jana droo ilichezeshwa kwa raundi ya nne ambayo itatimua vumbi tarehe 24/10/2016. Ratiba itakuwa hivi:
West Ham vs Chelsea
Manchester united vs Manchester city
Arsenal vs Reading
Liverpool vs Tottenham Hotspur
Leeds united vs Norwich
Newcastle vs Preston North end
Southampton vs Sunderland
Lakini utamu wa kombe ili ni kama umenogesha zaidi kwa maana timu kadhaa zilizopangwa kukutana zilishakutana katika ligi zao tayari kwa maana iyo inatazamwa kama je kisasi kinaweza kirudi?
Chelsea na West ham walikutana katika mechi ya kwanza katika ligi kuu ambayo ilichezwa siku ya jumatatu na Chelsea vijana wa Conte walishinda kwa goli 2-1, sasa swali je hao wagonga nyundo wanaweza kutumia mwanya wa kumsoma Chelsea katika mechi ya kwanza kumbamiza na kulivunja daraja?
Manchester united wakiwa chini ya Mourinho walikutana na Manchester city katika mchezo wa ligi kuu Uingereza na Man city walio chini ya Pep Guardiola wakashinda kwa mabao 2-1, sasa swali ni je Mourinho ataweza kulipiza kisasi?
Liverpool vs Tottenham ni mechi kali inayosubiriwa kwa hamu pia ni vita kati ya Klopp na Pochettino, katika mechi ya ligi kuu walipokutana walitoshana nguvu ya bao 1-1.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.