...Hii imetokea huko ujerumani ambapo daktari mmoja wa vichaa mwenye hospitali yake binafsi alikuwa anasafiri na vichaa
wake watatu wenye nafuu katika ndege ndogo toka mji mmoja kwenda mji mwingine.
Wakiwa hewani wagonjwa wawili walikuwa wanacheza cheza na kupiga kelele ndani ya ndege kwa nyuma wakati mmoja ametulia
kimya akiwa ameshika gazeti.
Kelele zilikuwa zinasumbua kiasi fulandi ndipo Yule mgonjwa aliyekuwa kimya akaenda kwa
daktari mbele katika chumba cha kuongozea ndege na kuzungumza na daktari wao
Mgonjwa: Samahani dokta, nilikuwa nafikiri kama tungewapa mipira wachezee ili wapunguze kelele
Daktari: Ni sawa haina tatizo, wazo zuri sana
Yule mgonjwa akarudi nyuma kwa wenzie kisha baada ya kama dakika kumi hivi kule nyuma kulikuwa kimya kabisa. Daktari
akafurahishwa mno na ubunifu wa yule mgonjwa mmoja na kuona kuwa maendeleo yake ni mazuri.
Daktari akataka kuwapa pongezi kwa kukaa kimya, akamuita yule mgonjwa aliyetoa wazo na kumuuliza
Daktari: aisee! Wazo lako ni zuri sana, waambie wenzio kuwa tukifika nitawapa zawadi kwa utulivu wa leo
Mgonjwa: nilipata wazo zuri zaidi ya lile, nilipowapa mpira nikawafungulia mlango wakachezee barazani. Wakiingia ndani
nitawaambia. Shukrani dokta.
Post a Comment
Post a Comment