Meneja wa sunderland ya uingereza David moyes ameshitakiwa na shirikisho la soka uingereza kwa utovu wa nidhamu aliouonesha jumatano timu yake ilivocheza na southampton.

Southampton walishinda mechi hiyo ya Kombe EFL Cup uwanjani St Mary's kupitia bao la Sofiane Boufa

Chama cha soka uingereza kilitoa ripoti hii "Moyes alitumia lugha ya kutusi au maneno ya kuudhi akiyaelekeza kwa mwamuzi wa mechi."

Kisa hicho kilitokea dakika ya 90 refa Chris Kavanagh alipokataa kuwapa Sunderland penalti baada ya mshambuliaji wa Sunderland Victor Anichebe kuonekana kuchezewa visivyo eneo la hatari.
Sunderland walilazwa 1-0.
Moyes, aliyeteuliwa meneja wa Paka Weusi Julai, ameshinda alama mbili pekee kutoka kwa mechi tisa ligini.
Amepewa hadi saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki Jumanne kujibu tuhuma hizo.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.