Droo ya kupanga makundi ya kombe la dunia 2018 yatakayofanyika uko nchini Urusi yatapangwa leo huko nchini Urusi katika jiji la Moscow.
Gwiji wa soka, Gary Lineker atasimamia shughuli hiyo akiwa kama mshehereshaji (MC) akiwa pamoja na mwandishi wa habari za michezo wa nchini humo mwanamama, Merry.
Fan ID
Moja ya vitu ambavyo mashabiki na watazamaji wa soka watakifaidi kutoka katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza mwakani mwezi wa juni ni kitu kinaitwa Fan ID (Kitambulisho cha shabiki) ambapo kitambulisho hicho kitamfanya shabiki wa soka kutoka nje ya Urusi ambaye ashafika nchini humo kwa ajiri ya kutazama michuano hiyo aweze kusafirishwa kutoka mahali alipo mpaka uwanjani bure. Ambapo kadi hiyo ya utambulisho imewekwa kihalali na nchi ya Urusi kwa ajili ya mashindano hayo.
 
Post a Comment
Post a Comment