Ulikuwa ni usiku mwengine mtamu wa ligi kuu Uingereza ambapo usiku wa leo kumechezeka michezo ya raundi ya 14.
Haya ndiyo yaliyotokea.
Salah afanya yake, Liver ikishinda 3-0
Mara baada ya kutokea benchi akichukua nafasi ya Dominic Solanke, nyota Mohammed Salah azidi kuwaonyesha watu na dunia ubora wake, na kwanini anaitwa Farao wa Misri mara baada ya kufunga tena magoli mawili na kufikisha magoli 12 katika ligi kuu, akizidi kukwea katika orodha ya wafungaji bora. Goli jengine la Liver lilifungwa na Sadio Mane.
Manchester city ni kama inakaribia kubeba EPL
Ni kweli bado mechi nyingi ili ligi kuu kuisha, bado michezo 24 lakini ni kama Manchester city hawaonekani kupotea tena ambapo leo usiku ilitegemewa labda wangeweza kupata suluhu mara baada ya Oriol Romeu wa Southampton kuchomoa goli dakika ya 76 baada ya kuwa nyuma toka Manchester city wafunge goli la kuongoza, goli likifungwa na Kevin De Bruyne.
Lakini baadae katika dakika tano za nyongeza, Raheem Sterling akaifungia Manchester city goli la ushindi na kuifanya kurudishwa pengo la alama 8 dhidi ya Man utd, inayoshika nafasi ya pili.
Giroud anapambana kurudisha heshima Arsenal
Ulikuwa ni usiku wa Arsenal mara baada ya kupata ushindi mnono dhidi ya klabu ya Huddersfield, ushindi wa 5-0 huku magoli yakifungwa na Alexzander Lacazette, Olivier Giroud aliyefunga mara mbili na Mesut Ozil.
Chelsea yapata ushindi mwembamba
Klabu ya Chelsea nayo ikapata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Swansea, goli likifungwa na Antonio Rudiger. Eden Hazard na Victor Moses wakianzia nje lakini pia Cesar Azpilicueta akikosa mchezo wa kwanza akiwa benchi chini ya kocha Antonio Conte. Amecheza michezo 51 akiwa chini ya Conte bila kufanyiwa mabadiliko.
Matokeo mengine.
Everton 4-0 West Ham
(Rooney akifunga mara tatu-Everton)
(Ashley Williams-Everton)
Bournemouth 1-2 Burnley
(C. Wood-Burnley)
(Brady-Burnley)
(J. King-Bournemouth)
Post a Comment
Post a Comment