Kuelekea kupangwa kwa makundi ya kombe la dunia yatakayoanza mwezi juni 2018, haya ndiyo unapaswa kuyajua kuelekea katika shughuli hiyo.
Wapi itafanyika;
State Kremlin wa jijini Moscow, Urusi ndio ukumbi ambao shughuli nzima ya upangwaji makundi utafanyika jioni ya leo ambapo una uwezo wa kuingiza watu 6000.
Muda wa shughuli;
Shughuli nzima imepangwa kuanza saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki ambao ni muda sawa na wa nchini Urusi.
Akina nani watahusika;
Mshambuliaji wa zamani wa Uingereza, Gary Lineker ndiye atahusika kama mshehereshaji mkuu akisindikizwa na mwandishi wa habari za michezo wa nchini Urusi Maria Komandnaya. Ambao nao watashirikiana na magwiji wengine kama mchezaji wa zamani wa Ufaransa, Laurent Blanc, gwiji wa Uingereza, Gordon Banks, Mbrazili Cafu, muitaliano Fabio Cannavaro, na nyota wa Uruguayi Diego Forlan, na mkali kutoka Argentina Diego Maradona, mlinzi wa zamani wa Hispania na Barcelona Carles Puyol pamoja na Nikita Simonyan kutoka Urusi.
Kuwa pamoja nami ntakujuza mengi kuhusu shughuli hiyo.
Post a Comment
Post a Comment