Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amemuhusia nyota wake Eden Hazard kama atataka kufikia mafanikio ya nyota kama Ronaldo na Messi basi inabidi awe na njaa ya kufunga na kufunga zaidi.
"Hazard anaweza kufikia rekodi na uwezo wa Ronaldo na Messi, ila tu inabidi awe na njaa ya magoli. Akifunga goli la kwanza basi apambane afunge na la pili, na akifunga la pili ahangaike afunge tena la tatu, inabidi awe na njaa ya magoli" alisema kocha Antonio Conte.
Ronaldo ametoka kushinda tunzo ya mchezaji bora ya Ballon d'or akiwapiku Lionel Messi na Neymar dos Santos huku Eden Hazard akimaliza kama mchezaji wa 19
Post a Comment
Post a Comment