Wababe wa ligi kuu Hispania, Real Madrid na Barcelona zimepanga kuivunja ligi kuu Uingereza kwa kuwang'oa wachezaji nyota wa klabu hizo za Uingereza.

Imeripotiwa kwamba kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane bado anamtaja Eden Hazard ambaye ni nyota wa Chelsea kwamba anamtazama kama chaguo lake la kwanza katika dirisha la usajili la mwezi januari.

Lakini wakati Zidane akiwaza hayo, uongozi wa Barcelona umepanga kuwanyakua nyota wa Chelsea, Cesar Azpilicueta na nyota wa Manchester united, Anthony Martial ambao wote inataka kuwasajili ili kujiimarisha zaidi ambao Barcelona imekuwa ikiingaika kuimarisha eneo lake la ulinzi haswa eneo la upande wa kulia ambapo toka Dani Alves aachane na klabu hiyo inaonekana kwa nafasi hiyo haijapata mrithi wa kuvaa viatu vya Dani Alves kwa usahihi.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.