Leo nakuletea orodha ya mawakala watano ambao hawajawai kumuacha mtu salama linapokuja suala la kutafutia wachezaji wao wapi pa kucheza huku wao wakipiga pesa ndefu bila hata kutumia nguvu kubwa.
Kazi kubwa ya mawakala ni kumsaidia mchezaji kujiunga na klabu fulani huku ye kama wakala akikamilisha mazungumzo yote kati ya timu na mchezaji na mwisho kuja kupata faida kama dalali.
Na hawa ndio walioongoza katika orodha hiyo ya mawakala waliofanya biashara sana mwaka 2017.
5. Volker Struth
Huyu anashika namba 5 katika orodha hii ambapo makao yake kajichimbia sana Ujerumani ambapo yeye ndiye aliyesaidia usajili wa Marco Reus kutoka Borrusia Monchlebragh na kujiunga na Borrusia Dortmund.
Struth anamiliki wachezaji: 88
Mastaa anaowamiliki: Toni Kroos, Marco Reus, Benedikt Howedes, Omer Toprak, Gonzalo Castro na wengine
Kiasi alichoingiza: $34.3milioni
4. Mino Raiola
Huyu anafahamika na wengi kutokana na machachari yake akiwa ni raia wa Italia.
Huyu jamaa alifahamika zaidi mara baada ya kuhusika katika usajili wa mchezaji wa zamani raia wa Jamhuri ya Czech, Paul Nedved ambapo yeye Raiola alihusika kumtoa nyota huyo kutoka Sparta Prague na kumpeleka Juventus kisha kumaliza Lazio.
Lakini pia anatambulika zaidi alipopiga hela ndefu katika usajili wa Paul Pogba alipotoka na kurudi Manchester utd.
Kocha wa zamani wa Manchester utd, Sir Alex Ferguson aliandika kwenye kitabu chake kwamba kama kuna mawakala wawili anaowachukia na hapendi kuwaona basi ni Mino Raiola.
Raiola anamiliki wachezaji: 55
Mastaa anaowamiliki: Paul Pogba, Romelu Lukaku, Blaise Matuidi, Henriky Mkhitaryan, Marco Verratti na wengine.
Kiasi alichoingiza mwaka 2017: $43.5milioni
3. Jonathan Barnett
Huyu jamaa ana uhalisia wa Uingereza ambapo jamaa katika kucheza kwake bingo alifanikiwa kupiga kiasi kikubwa cha pesa alipofanikiwa kukamilisha usajili wa Gareth Bale kutoka Tottenham Hotsupr.
Lakini pia jamaa katika mwaka huu amehusika katika usajili wa kiungo Glyfi Sigurdsson aliyekuwa anaichezea Swansea ingawa kwa sasa yupo Everton.
Barnett anamiliki wachezaji: 116
Mastaa anaowamiliki: Gareth Bale, Glyfi Sigurdsson, Adrien Silva, Adam Lallana, Joe Hart, Luke Shaw na wengine kibao.
Kiasi alichokitengeneza mwaka 2017: $53.4milioni
2. Jorge Mendes
Huyu ndio anatajwa kuwa wakala bora zaidi ambapo ameshawai kushinda tunzo nyingi kama wakala bora zikiwemo tunzo tatu za FIFA.
Jorge Mendes ni raia wa Ureno na ametambulishwa sana duniani baada ya kuhusika na watu wenye nguvu sana ambao wapo chini yake. Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho ambao wote walitambulishwa katika dunia ya soka na huyu jamaa.
Cristiano Ronaldo alipotoka Sporting Lisbon na kwenda Manchester utd na kwenda tena Real Madrid jamaa huyu ndio alihusika.
Jose Mourinho kutoka FC Porto kuja kuipa mataji Chelsea, basi huyu jamaa nae alihusika.
Mendes anawamiliki wachezaji: 102
Mastaa anaowamiliki: Cristiano Ronaldo, Angel Di Maria, James Rodriguez, Diego Costa, Bernardo Silva, Jose Mourinho na wengine kibao.
Kiasi cha pesa alichotengeneza mwaka 2017: $76.9milioni
1. Constantin Dumitrascu
Jina lake ni geni maskioni mwa wengi lakini ndiye aliyepiga pesa ndefu mwaka huu kwa mawakala akitangazwa na jarida la Forbes.
Usajili wa Edinson Cavani kutoka Napoli kujiunga na PSG basi jamaa huyu alihusika kama dalali.
Dumitrascu anawamiliki wachezaji: 87
Mastaa anaowamiliki: Edinson Cavani, Phillipe Coutinho, Douglas Costa, Nemanja Matic, Dimitri Payet, N'golo Kante, Raphael Varane, Olivier Giroud na wengine kibao.
Kiasi alichotengeneza mwaka 2017: $107.8milioni

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.