Michael Emenalo ambaye siku kadhaa aliandika barua kwa uongozi wa klabu ya Chelsea kuomba kujihudhuru huenda akapatikana mtu wa kumrithi kwa haraka na pengo lake kuzibwa haraka.

Kuna wengi wanatajwa katika kuchukua nafasi yake wakiwemo wachezaji wa zamani wa klabu hiyo Frank Lampard na Didier Drogba ambaye kwa sasa ni mchezaji na mmiliki wa klabu ya Phoenix ya nchini Marekani.
Lakini inaelezwa pia Marina Granovskaia ambaye ni mmoja wa mabosi wa klabu hiyo akiwa kama msaidizi wa mmiliki wa klabu hiyo mrusi, Roman Abramovich.
Lakini pia jina linaloonekana kuweza kuziba pengo la Emenalo kwa maono ya mmiliki mwenyewe anatazamia kibarua hicho kumpatia kocha wa sasa wa klabu ya Hull City, Leonid Slutsky ambaye naye ni mrusi huku akitajwa kuaminika sana na mmiliki wa klabu huyo na kwa taarifa zilizopo ni kwamba kocha huyo yupo jijini London katika moja ya hoteli iliyopo mitaa ya Stamford Bridge ambapo ndipo panapatikana uwanja na ofisi za klabu ya Chelsea.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.