Siku ya leo katika ligi kuu Tanzania Bara kutakuwa na mchezo mmoja wa ligi hiyo ambapo Simba SC itashuka uwanjani kumenyana na klabu ya Lipuli katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Simba itahitaji kushinda mchezo huu wa leo ili izidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ambapo jana klabu ya Yanga Africa ilitoka suluhu na kushindwa kumshusha Simba kutoka kileleni.
Simba ina alama 22 katika msimamo wa ligi kuu ikiwa imeshacheza michezo 10 wakati kama jana Yanga angeshinda basi angepanda kileleni na kuongoza ligi kuu kwa kupata alama 23 ikiwa na michezo 11 lakini kutokana na matokeo ya 1-1 yanaifanya klabu hiyo ya Jangwani kuendelea kushika nafasi ya tatu ukiwa na alama 21 ikiwa na michezo 11 wakati nafasi ya pili inashikwa na Azam FC yenye alama sawa na Simba, alama 22 ikiwa na michezo 10.
Matokeo ya michezo ya jana katika VPL;
Post a Comment
Post a Comment