Mshambuliaji raia wa Argentina anayeichezea klabu ya Barcelona, Lionel Messi ambaye siku kadhaa nyuma alishinda tunzo ya mfungaji bora wa Ulaya na ligi kuu Hispania, La Liga kwa msimu wa 2016-2017 amempiga dongo Neymar ambaye alikuwa mchezaji wa Barca kabla ya kuungana na PSG katika dirisha kubwa la usajili na kuweka rekodi ya mchezaji ghali kwa kiasi cha paundi milioni 198.

Messi alipohojiwa alisema "Kuondoka kwake (Neymar) kimeidhoofisha timu kwenye ushambuliaji lakini katika nafasi ya ulinzi imetuhimarisha zaidi" akimaanisha kuwepo kwa Neymar klabuni hapo kulikuwa kunaifanya klabu ishambuliwe na kufungwa zaidi.

Barca mpaka sasa haijaruhusu kufungwa goli katika michezo 13 ambapo imecheza bila Neymar wakati Messi akifunga magoli 16 katika mashindano yote.

Barcelona leo inashuka dimbani kumenyana na Valencia ambayo imekuwa na msimu bora huku ikishika nafasi ya pili katika msimamo wa La Liga huku Neymar akiiongoza PSG kumenyana na AS Monaco ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Ufaransa maarufu kama Ligue 1.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.