Mshambuliaji nyota wa zamani ambaye alishawai kuzitumikia klabu kama Manchester city, Real Madrid na AC Milan, Robinho ambaye kwa sasa anaandamwa na majanga ya hukumu ya kesi inayomkabili ya ubakaji ambapo hukumu ilifanyika na nyota huyo kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa.

Lakini huenda nyota huyo ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya nchini Brazil, Atletico Mineiro akaiepuka kesi hiyo.

Ndiyo huenda kifungo hicho kikamkosa mara baada ya kuelezwa sheria za nchini Brazil huenda zikamlinda na ikatokea kimojawapo, akapunguziwa kifungo au kesi ikafutwa kabisa kutokana na nyota huyo kuwa na haki ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama ya nchini ya Italia ambako huko ndiko kunaelezwa nyota huyo alifanyia tukio hilo la ubakaji.

Nchi ya Brazil ina sheria ya kuwalinda wananchi wake dhidi ya kesi zinazowakabili nje ya nchi yao, na huwa inakuwa na uangalizi mkubwa kwa mwananchi wao kufungwa jela nje ya nchi yao.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.