Leo ni siku nyengine ambapo macho ya watu zaidi ya bilioni moja duniani kote yatakuwa barani Ulaya kutazama michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Hapa nakuletea michezo itakayovuta hisia za watu wengi.
1. FC Basel vs Manchester united
Sio kama mchezo huu utatazamwa sana kutokana na ushindani katika kundi lao ili kufuzu, ila utakuwa na mvuto kutokana na wengi kutamani kuona je Pogba na Ibrahimovic watayafanya makubwa kama walivyoyafanya katika mchezo wa ligi kuu uliopita dhidi ya Newcastle, huku wakirudi kutoka kwenye majeruhi.
Mchezo huu unategemewa kutokuwa na ushindani sana, katika kugombania nafasi ya kufuzu kwa vile Manchester united inahitaji alama moja tu ili ijihakikishie kufuzu.
2. Atletico Madrid vs AS Roma
Mchezo huu utatazamwa sana kutokana na ukubwa wake lakini pia kutokana na Atletico kugombani kufuzu katika hatua ya 16 bora. Ingawa pia AS Roma amekuwa na msimu mzuri wakati katika kundi lao, kundi C, Roma ndio inaongoza kundi ikiwa na alama 9 ikifuatiwa na Chelsea yenye alama 8 wakati Atletico ina alama 6.
Kwa upande wa Atletico Madrid ambayo imekuwa haina matokeo ya kuridhisha, ili iweze kufuzu itahitaji kushinda mchezo wa leo na mchezo utakaofata ambao utakuwa dhidi ya Chelsea, lakini tu kama Chelsea akipoteza leo dhidi ya Qarabag.
3. Paris St. Germain (PSG) vs Celtic
Hauonekani kuwa mchezo mgumu kwa PSG ukizingatia kwenye kundi lake tayari ishafuzu kucheza hatua ya 16 bora ikiwa na alama 12.
Kwa Celtic itakuwa ngumu kwake kutoboa katika mchezo huu, kutokana na safu ya ushambuliaji ya PSG kuwa tamu.
Kinachoubeba mchezo huu kuwa mtamu ni kutokana na safu ya ushambuliaji ya PSG inayoongozwa na Neymar, Cavani na Kylian Mbappe ambapo utamu wa mchezo huu unaweza kuwa kutokana na magoli mengi.
4. Juventus vs Barcelona
Klabu ya Juventus iliwapumzisha nyota wake katika mchezo wa ligi kuu ikitegemea kuwatumia katika mchezo huu wakati FC Barcelona ikishuka katika mchezo huu ikitaka kushinda ili kujihakikishia kufuzu kucheza katika hatua ya 16 bora.
Lakini Juventus na wao watataka kupambana ili nayo kujiweka sawa kuweza kufuzu.
Ni kama marudio ya fainali ya ligi ya mabingwa iliyochezeka mwaka 2015 na Barcelona kutwaa taji hilo.
Mchezo huu utabebwa kutokana na ukubwa wa timu zote mbili ingawa Juventus amekuwa hana mfululizo mzuri wa ushindi katika michezo iliyopita.
5. Anderlecht vs Bayern Munich
Mchezo mwengine ambao huenda ukazalisha magoli mengi usiku huu. Bayern Munich bado anahitaji kushinda ili afuzu kucheza hatua ya 16 bora.
Utamu wa mchezo utakuja pale ambapo Anderlecht atataka kumkazia Bayern ili kutokuonyesha unyonge wakati kwa upande wa Bayern atakuwa anauangalia mchezo huu kama mchezo muhimu kwake kufuzu.
6. Qarabag vs Chelsea
Jana kocha wa Chelsea, Antonio Conte alipohojiwa kuhusu mchezo huu alisema anautazama mchezo huu kama mchezo mgumu zaidi kuliko mchezo wowote kutokana na uhitaji wa Chelsea kufuzu katika mchezo huu ikiwa na alama 8, ikifukuziwa na Atletico Madrid.
Ili Chelsea afuzu kucheza hatua inayofata hana budi kushinda mchezo wa leo wakati kwa Qarabag atakuwa anapambana ili kuonyesha ukubwa wake ukizingatia pia mchezo huu utachezewa uwanjani kwao nchini Azbearjan.
Michezo mingine;
CSKA Moscow vs Benfica
Sporting CP vs Olympiacos

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.