Nyota wa klabu ya Chelsea ambaye ni raia wa Ubelgiji, Thibaut Courtois huenda akatimkia Real Madrid mara baada ya kuongea leo mchana katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya Qarabag.

Courtois ambaye amekuwa akihusishwa na kutakiwa na Real Madrid aliulizwa kuhusu kuongeza mkataba wake na klabu yake ya sasa ambapo mkataba wake unaisha msimu ujao.

"hakuna mazungumzo yanayoendelea kati yangu na klabu (Chelsea) na hata kama yapo basi inabidi yafanyike na wakala wangu lakini kwangu mimi nachoangalia ni michezo inayofata" alisema Thibaut Courtois.

Courtois amekuwa akikaririwa mara kadhaa akisema anayakumbuka maisha ya jiji la Madrid ambapo huko alishawai kuichezea klabu ya Atletico Madrid inayopatika Madrid na katika hilo kuhusishwa na timu ya Real Madrid inayotokea hukohuko mji wa Madrid basi wachambuzi wanasema huenda kwa majibu ya Courtois kuhusu kuongeza mkataba ndani ya Chelsea kuonekana kama hayapo moja kwa moja basi labda huenda anataka kutimkia Madrid.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.