Kiungo Mkongwe wa Arsenal Muhispania Cazorla,ilibakia kidogo tu akatwe mguu wake wa kulia na kupelekea mwisho wake wa kucheza soka
Cazorla ambaye hajawahi kukanyaga kwenye dimba la mpira tangu mwezi wa kumi mwaka jana alipo pata majeraha kwenye ankle yake alipokuwa wakicheza na Ludogorets.
Baada ya kupata majeruhi hayo,kocha wenger alijua kuwa Cazorla anaweza akawa nje kwa wiki kadhaa tu na sio miezi kama ilivyo sasa.Mpaka sasa cazorla kafanyiwa oparesheni 8 kwenye mguu wake wa kulia ambapo zilipelekea madaktari kumwambia kuwa hataweza kucheza mpira tena maishani mwake.
Pia Cazorla alipata ugonjwa unaitwa Gangrene katika kifundo chake hicho cha jeraha.Ugonjwa huu maana yake ni kufa kwa seli damu hasa sehemu yenye jeraha kwa sababu ya kukosa hewa ya oxygen.
Gangrene hiyo ilipelekea kukatwa kwa semtimita kadhaa za kifundo chake ili kuzuia ugonjwa usitapakae Baada ya operesheni hiyo,Cazorla alikatwa sehemu ya nyama ya mkono wake ili ukazibe mguuni.Kwa hiyo sehemu ya tatoo ya kazorla iliyokuwa mkononi sasa inaonekana mguuni mwake.
Anatarajiwa kurudi mazoezi Mda si mrefu

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.