Mshambuliaji wa Manchester utd ambaye ni rai wa Ubelgiji, Romelu Lukaku amewajibu wale wote wanaombeza juu ya ukame wake kupachika magoli mara baada ya kutokufunga katika michezo 6 ya michuano yote.


Mchezo wa mwisho kwa mshambuliaji huyo kuifungia klabu yake ulikuwa dhidi ya Crystal palace ambapo mbaada ya hapo hajawai kuifungia tena timu yake hiyo.

Katika kipindi cha Super Sunday ambacho huwa kinarushwa na Sky Sports ambapo Lukaku alikuwa akifanya mahojiano na nyota wa zamani raia wa Ufaransa, Thierry Henry, Lukaku alisema "mimi bado ni kijana mdogo, nina miaka 24. Kusemwa kwangu juu ya kutokufunga sio sawa, nachotazamia kwa sasa muhimu ni timu yangu ishinde nami hata nisipofunga sio tatizo"

Lukaku ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi kikosini hapo kwa sasa akiwa amesajiliwa akitokea Evertona mabpo aliigharimu Man utd kiasi cha paundi milioni 75 ameifungia klabu hiyo mabao 11 katika michezo 11 aliyoichezea klabu hiyo.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.