Kocha mwenye maneno mengi, Jose Mourinho asubuhi ya leo amehudhuria kesi yake nchini Hispania katika mahakama ya Pozuelo de Alcoron ambayo ipo karibu na jiji la Madrid inapopatikana klabu ya Real Madrid ambayo alishawai kuifundisha hapo nyuma.

Mourinho ambaye ni kocha wa Man utd kwa sasa ana kesi ya kukwepa kodi pindi alipokuwa anaitumikia klabu hiyo ya Real Madrid ya nchini Hispania na subuhi ya leo alifika kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Mourinho jana mchana aliipiga dongo klabu ya Real Madrid ambayo alishawai kuifundisha mara baada ya klabu hiyo kupokea kichapo kutoka kwa klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo jumamosi iliyopita Mourinho aliiongoza klabu yake ya Man utd na kuibamiza klabu hiyo.

Mourinho alisema "Tottenham ilimpiga Liverpool magoli 4-1, imempiga Real Madrid 3-1 na ameshindwa kupata goli lolote kwangu, wachezaji wangu wanahitaji pongezi"

Mourinho ataiongoza klabu yake ya Manchester utd kumenyana dhidi ya Chelsea ya Antonio Conte kocha ambaye walishawai kutupiana maneno wiki kadhaa nyuma mara baada ya kocha Antonio Conte kulalamika kuhusu majeruhi katika klabu yake. Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Stamford Bridge ambapo msimu uliopita Mourinho alishuudia akikandamizwa mabao 4-0 na klabu hiyo. Mchezo huo utachezwa jumapili hii saa moja usiku.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.