Kuna fununu zinaendelea juu ya hatima ya nyota Cristiano Ronaldo ndani ya klabu yake ya Real Madrid. Taarifa zikieleza nyota huyo analazimisha kuondoka klabuni hapo akiwa anamshawishi mmiliki wa klabu hiyo Frorentino Perez aweze kumuuza ingawa mmiliki huyo amesema hapana, akitumia kithibitisho cha muda uliobaki kwa nyota huyo katika mkataba wake na klabu hiyo. Ambapo amebakiza mkataba unaoisha 2021.
Habari zinasema, Ronaldo anaona ameshapoteza heshima aliyokuwa nayo mwanzo mara baada ya klabu yake kumfukuzia winga aliyekuwa AS Monaco ambaye baadae aliuzwa kwenda PSG, Kylian Mbappe.
Ronaldo anaona kwa Madrid kumtaka Mbappe inamaanisha huyo ndio alikuwa anaandaliwa kuwa mfalme mpya klabuni hapo na ilishakubali kutoa kiasi cha paundi milioni 140 ili kumsajili nyota huyo ambaye baadae alitimkia PSG.
Inaelezwa pia maboss na viongozi wa Real Madrid wanatumia kipengele cha miaka aliyobakisha nyota huyo katika mkataba wake kama kipengele cha kumzuia kuondoka na huku kiasi cha pesa kinachoweza kumtoa nyota huyo klabuni hapo kikiwa ni Euro milioni 1,000 ambalo ni dau kama mara 5 alilonunuliwa nyota aliyeweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi Neymar akitokea Barcelona na kujiunga na PSG.
Lakini pia kuhusishwa kwa Neymar kujiunga na Real Madrid akitokea PSG ambapo kuna fununu zinaeleza nyota huyo hana furaha ni kama kumezidi kumtibua Ronaldo akiamini kama Madrid ikifanikiwa kumsajili Neymar basi ye hatokuwa na chake klabuni hapo kutokana pia na umri kuanza kumtupa mkono.
Post a Comment
Post a Comment