Kocha wa Manchester city raia wa Hispania, Pep Guardiola amefanya mkutano na waandishi wa habari kuelekea wiki nyengine ya ligi kuu Uingereza.
"Nataka tu kuwataadharisha wapinzani kwamba haya tunayoyafanya bado tunapambana kuyafanya zaidi, wasifiri tukajisahau tukazembea" ndio kauli kubwa aliyoiongea kocha huyo akitamba kwa kusema bado atafanya makubwa.
Pep Guardiola mpaka sasa hajafungwa mchezo hata mmoja na akiiongoza vizuri Man city kuifunga Arsenal wiki mbili zilizopita. Huku akiwa kileleni kwa tofauti ya alama 8 dhidi ya Man utd inayoshika nafasi ya pili.
Man city itamkosa Otamendi kuelekea katika mchezo huo dhidi ya Leicester wiki hii lakini Aguero anatajwa kuwepo kwenye kikosi kitakachoivaa 'The Foxes'.
Kocha Guardiola jioni ya leo alitangazwa kuwa kocha bora wa mwezi Oktoba na huku Leroy Sane akiwa mchezaji bora wa mwezi huo.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.