Klabu ya Barcelona ipo kwenye mazungumzo na wakala wa nyota wa Arsenal, Mesut Ozil ili kumsajili nyota huyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi januari katika dirisha dogo.
Ozil anatajwa kuwepo sokoni mara baada ya nyota huyo kugoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Arsenal iliyomsajili akitokea Real Madrid na sasa wakala wake ameanza mazungumzo na Barcelona iliyosema ipo tayari kutoa kiasi cha Euro milioni 20 ambazo ni sawa na paundi milioni 17. Ambacho ni kiasi kidogo ingawa Arsenal huenda wakakubali kukipokea maana mchezaji huyo amebakisha miezi kadhaa tu kumaliza mkataba wake na washika bunduki ambapo inaelezwa mwezi wa sita mwakani ndio mkataba huo unaisha.
Post a Comment
Post a Comment