Mshambuliaji wa klabu ya Everton ya nchini Uingereza, Oumar Niasse ambaye ni raia wa Senegal amewekwa chini ya uangalizi na chama cha soka nchini Uingereza, FA mara baada ya tuhuma anazotuhumiwa kujiangusha katika mchezo dhidi ya Crystal Palace ambapo uliisha kwa suluhu ya 2-2.
Niasse katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Crystal Palace alijiangusha ndani ya eneo la hatari la Crystal na kumfanya mwamuzi Taylor kuikubali kuwa penati na Leighton Baines akapiga tuta na kushinda.
Mwanzoni mwa msimu kabla kuanza kwa ligi kuu chama cha soka nchini Uingereza kilieleza nia yake ya kupunguza kujiangusha kwa wachezaji, na kama mchezaji angelalamikiwa basi chama hicho kingemfanyia uchunguzi na kama ingebainika kwamba ni kweli basi mchezaji huyo angeazibiwa.
Sasa rungu hilo huenda likaanza kwa Niasse endapo uchunguzi ukionesha ni kweli alijiangusha.
Post a Comment
Post a Comment