Barani Ulaya ndipo kunapoelezwa kushamiri zaidi kwa mashabiki wa soka na hata pia mashabiki wengi wa soka duniani wanafatilia soka la barani humo. Kwa maana hiyo kunakuwa na msukumo mkubwa haswa kutoka kwa mashabiki pale timu inapofanya vibaya, haswa timu hiyo ikiwa ligi kuu, na kwa hivyo mzigo wa lawama huwa unamdondokea kocha hata kama aliipatisha mafanikio klabu hiyo muda mfupi nyuma, angalia kilichomtokea Claudio Ranieri pale Leicester, alipandisha daraja, akainusuru isishuke daraja na akaipatia taji la kwanza la ligi kuu nchini Uingereza. Lakini hayo yote hayakuonekana pale timu ilipokuwa na mfululizo wa matokeo mabovu, wakamtimua bila kumwangalia usoni.
Mara baada ya aliyekuwa kocha wa West Bromwich, Tony Pulis baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa muda mrefu, akiifundisha jumla ya michezo 106 na kufunga 105 lakini kocha huyo katimuliwa baada ya kipigo cha jumamosi dhidi ya Chelsea cha 4-0.
Leo kocha wa klabu ya ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A, Udinese Calcio anayeitwa Luigi del Neri naye ametimuliwa na klabu yake mara baada ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Cagliari.
"Tunapenda kutangaza kuachana na kocha Luigi del Neri na tunashukuru kwa yote aliyoyafanya na klabu yetu kwa muda wote huo (miezi 13)" alisema mmoja wa wakilishi wa bodi ya Udinese.
Kocha anayetajwa kushika nafasi ya kocha huyo ni Massimo Oddo.

Post a Comment
Post a Comment