Ni usiku wa mabingwa, ni usiku wa wababe barani Ulaya ambapo vigogo barani Ulaya vitashuka viwanjani kugombania nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora. Viwanja mbalimbali vitatimua vumbi lakini hapa nakuletea baadhii ya michezo itakayovuta hisia za watu wengi usiku wa leo na kama utataka kubashiri au kubeti katika michezo hii inabidi utulize akili sanaa kutokana na ugumu wa michezo hii.
Borrusia Dortmund vs Tottenham (Kundi H)
Mchezo huu unaleta utamu pale ambapo Dortmund atatamani ashinde ili arudishe matumaini ya kufuzu katika hatua ya 16 bora, lakini uwezekano wake wa kufuzu kuvuka hatua hiyo ni pale tu Real Madid ambaye wapo kundi moja atakapopoteza mchezo wake dhidi ya APOEL Nicosia. Ambapo kwa Tottenham tayari ashafuzu kwa maana hiyo huenda mchezo huu hatotaka kujisumbua kutumia akili nyingi, lakini pia anaweza kupambana kutokana na kutotaka kumaliza mtu wa pili kwenye kundi lake ili atakapofika hatua ya 16 bora akutane na aliyemaliza nafasi ya pili katika kundi jengine.
Msimamo wa kundi lao upo hivi;
1. Tottenham ana alama 10
2. Real Madrid ana alama 7
3. Borrusia Dortmund ana alama 2
4. APOEL Nicosia ana alama 0
(wote wakiwa wamecheza michezo 4)
Monaco vs RB Leipzig (Kundi G)
Moja kati ya michezo migumu zaidi usiku wa leo, japo wengi wanauchukulia poa lakini kiukweli ni mchezo ambao huenda ukawa na soka gumu la kushambuliana kila wakati.
Monaco hana cha kupoteza, ili afuzu kucheza kombe la dunia iitambidi apambane kwa kila mchezo na apate ushindi ili aweze kufuzu, lakini ana nafasi finyu sana kufuzu kutokana na alama alizokuwa nazo itabidi walioko juu yake yaani FC Porto na RB Leipzig wote wapoteze michezo yao, lakini nayeye ashinde mchezo huu wa leo na ule unaofta dhidi ya FC Porto.
Msimamo wa kundi lao upo hivi;
1. Besktas ana alama 10
2. FC Porto ana alama 6
3. RB Leipzig ana alama 4
4. Monaco ana alama 2
Napoli vs Shakter Donetsk (Kundi F)
Huu nao ni mchezo mwengine ambapo hapa kibarua anacho Napoli ambapo yeye anashika nafasi ya 3 akiwa na alama 3 huku Shakter anashika nafasi ya pili akiwa na alama 9.
Ugumu wa mchezo huu unakuja pale ambapo Napoli anahitaji ushindi katika mchezo huu ili afikishe alama 6 ambapo katika mchezo wa mwisho atakutana na kibonde wa kundi hili Feyernood ambaye yeye hana alama hata moja wakati kama kwenye mchezo huo, Napoli akishinda atajipa asilimia 50 za kufuzu kucheza hatua inayofata lakini tu kama Shakter akifungwa na kiongozi wa kundi hilo Manchester city ambaye yeye huenda asitumie nguvu kubwa kupambana kutokana na tayari ashafuzu akiwa mna alama 12.
Msimamo wa kundi hili;
1. Manchester city ana alama 12
2. Shakter Donetsk ana alama 9
3. Napoli ana alama 3
4. Feyernood ana alama 0
Sevilla vs Liverpool (Kundi E)
Kama unatakiwa kuwa makini usiku wa leo, basi katika mchezo huu ndio inatakiwa utulize akili kama unataka kuubashiri au kama unataka kupata radha ya soka, radha ya mpira wa kushambuliana basi angalia mechi hii. Ni mechi ngumu ambayo naweza kusema ni zaidi ya fainali kutokana na nafasi zao timu hizo katika kundi lao. Sevilla akiwa nyumbani anatakiwa apmabane kwa nguvu zake zote ili amshushe KLiverpool katika kilele alichokaa katika kundi hili, lakini pia Liverpool mwenye mfululizowa mechi atataka apate ushindi ili ajiweke salama kule kileleni. Yaani kama mmoja akipoteza katika mchezo huu basi naweza kusema akaaga mashindano ya ligi ya mabingwa. liverpool amnaongoza kundi akiwa na alama 8 huku akifatiwa na Sevilla mwenye alama 7, alama moja tofauti na Liverpool. Wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Spartak Moscow mwenye alama 5 ambaye yeye anacheza dhidi ya Maribor, kibonde katika kundi hili.
Lakini pia utami wa mchezo huu unanogeshwa palea mabpo timu hizi zilipokutana katika mchezo wa fainali ya kombe la Europa League mwaka 2016 na Sevilla kuweka rekodi ya kulibeba taji hilo mara tatu mfululizo, kwa hiyo huenda Liver akaingia katika mchezo huu akitaka kulipiza kisasi ingawa mchezo wa kwanza wa makundi katika klabu bingwa uliisha kwa suluhu ya 2-2.
Msimamo wa kundi lao;
1. Liverpool ana alama 8
2. Sevilla ana alama 7
3. Spartak Moscow ana alama 5
4. Maribor ana alama 1
Michezo mingine itakayochezwa leo;
Spartack Moscow vs Maribor (kundi E)
Manchester city vs Feyernood (kundi F)
Besiktas vs FC Porto (kundi G)
APOEL Nicosia vs Real Madrid (kundi H)





Post a Comment
Post a Comment