Kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Mesut Ozil ametoa neno kuhusu taarifa zilizogaa kuhusu kuikacha klabu yake ya sasa na kujiunga na Man utd.

Ozil ambaye alisajiliwa na Arsenal akitokea Real Madrid amesema hapendezewi na mpango wa kujiunga na wababe hao wa Manchester na badala yake bado anaendelea kubaki Arsenal.

"Mi ni mchezaji wa Arsenal kwa asilimia 100 na nina furaha kuwa hapa, nadhani suala la kutoka hapa ni la kuliongelea baadae lakini kwa sasa ninabaki kuwa hapa" alizungumza Ozil huku kukielezwa kwamba nyota huyo aligoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Arsenal.

Lakini pia kuna taarifa zilikuwa zinadai kwamba Arsenal wapo tayari kumuuza nyota huyo huyo ili kupata fedha kuliko kumwacha mchezaji huyo aondoke bure kipindi cha kiangazi, mwezi juni ambapo ndipo mkataba wake utakapoisha.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.