Usiku wa leo kutakuwa na mchezo mmoja wa ligi kuu Uingereza maarufu kama Premier League ambapo utawakutanisha timu ambazo zinagombani nafasi ya katikati, yaani zenyewe zinataka kama kwa mafanikio basi ni kucheza mashindano ya Europa League, nazizungumzia Brighton & Hove Albion dhidi ya Stoke city vijana wa Mark Hughes, klabu ikimilikiwa na mmiliki wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Bet365.
Lakini usiku wa leo hawatakuwa Brittania Stadium uwanja wa zamani wa Stoke city ambao umebadilishwa jina na sasa unaitwa Bet365 Stadium ila watakuwa wageni wa Brighton, uwanja wa The Amex stadium.
Utamu wa mchezo huu unakuja pale klabu hizi zinapogombani nafasi ya juu ambapo ikiwa Stoke city atashinda mchezo atafikisha alama 15 ambapo apo atakuwa sawa na Brighton ingawa ili amshushe Brighton iliyoko nafasi ya tisa inabidi Stoke city yenye nyota kama Chicharito, Pablo Zabaleta na Joe Hart inabidi washinde kwa tofauti ya magoli 9 yaani kama Stoke anataka amshushe Brighton, inabidi amfunge 9-0, au 10-1 au hata 11-2.
Tusubiri tuone, lakini kizuri mchezo huu utaonyeshwa mubashara (live) humuhumu.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.