Ronaldo de Assiss Moreira ndilo jina lake kamili ingawa anafahamika zaidi kama Ronaldinho Gaucho jina ambalo wengi wetu tulikuwa tunapenda sana kuliskia haswa tukiwa vibanda umiza huku joto kalii likitunyonya, ila kutokana na mauwezo ya jamaa na utamu wake katika soka alikuwa anatusahaulisha lile joto la mule ambalo kama ungeweka maji kwenye sufuria bila kuwepo kwa moto ungekuta tu maji yanachemka.

Nirudi kwenye maada kuu.
Jamaa huyo ninamshtaki kwa kuwa mchoyo katika kipindi chake wakati anacheza mpira, uchoyo dhidi ya vijana kama sisi tuliozaliwa miaka ya  karibia 2000 ametunyima uhondo sana yani anakuja kutoka kwenye anga la soka la kiushindani huku sisi tukiwa bado hatujaelewa maana ya soka. Hatujamjua vizuri jamaa alikuwa nani, unazani ukimwelezea yule kijana aliyezaliwa miaka ya 2000 kuhusu Gaucho a.k.a Minjino atakupa historia sawa na yule aliyeshuhudia michuano ya kombe la dunia 2002 kule Japan, Phillipe Scolari aliyekuwa kocha wa Brazil miaka hiyo akimkataa Romario aliye kwenye ubora wake akamchukua Gaucho? hawezi kutoa historia sawa.

Hebu fikiria, mtoto aliyezaliwa mwaka 2000 mpaka aje autambue mpira na aweze kupata ruhusa ya kuangalia mpira na auelewe ni kama miaka 12 ambapo ni sawa na mwaka 2012 baadae wakati Ronaldinho anaondoka Ulaya akiwa kwenye klabu ya Ac Milan ukiwa ni mwaka 2011 miaka 31 toka azaliwe.

Lakini tatizo sio la wazazi waliomzaa kijana huyo miaka ya 2000 ila tatizo na kosa kubwa alilifanya Ronaldinho mwenyewe.

Kwanini alithamini sana starehe na kutunyima utamu wake wa soka? kwanini hakusubiri aondoke katika soka la Ulaya akiwa ata na miaka 40? sio kwamba alichoka, ila kwa vile alikuwa mchoyo juu ya watoto wa 2000 hakuwathamini. Ni kweli kuna video nyingi mtandaoni lakini utamu wa soka uushuhudie kule juu upande wa kushoto au wa kulia wa TV kuwe kumeandika neno 'LIVE' hapo ndio utamu ule ambao haujachakachuliwa unapotokea.

Leo tunamshtaki Ronaldinho a.k.a Minjino kwa kutunyima utamu wa soka ikiwa aliondoka kwenye soka la Ulaya akiwa na miaka 31 tu, yaani alikuwa ni kama umri sawa na Messi au Ronaldo wa sasa.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.