Leo tunakuletea msimamo wa klabu za ligi kuu Uingereza ulivyo kulingana na watu wanavyozifatilia (followers) katika mitandao ya kijamii haswa mtandao wa Instagram.
NB; Takwimu hizi ni kutokana na kurasa rasmi za klabu hizo zilivyofatiliwa na mashabiki duniani.
()=Ni nafasi ya klabu hiyo katika msimamo wa ligi kuu Uingereza.
K=×1,000
M=×1,000,000
20. Huddersfield (10)
Wafuasi; 50.2K
Klabu hii ndio klabu yenye wafuasi wachache zaidi katika timu za ligi kuu Uingereza katika mtandao huo wa Instagram. Lakini ufinyu huo huenda umetokana na uchanga wa timu hiyo katika ligi kuu.

19. Brighton & Hove Albion (8)
Wafuasi; 70K
Hii nayo bado ina ugeni katika ligi ambapo huenda hiyo ikasababisha kutokuwa na wafuasi wengi katika mtandao huu.

18. Newcastle (11)
Wafuasi; 119K
Ikiwa chini ya kocha Rafa Benitez, anaiongoza vizuri klabu hiyo katika ligi kuu lakini katika mtandao wa Instagram haina makali ikishika nafasi ya 3 kutoka mwisho kwa kuwa na wafuasi wengi.

17. Burnley (7)
Wafuasi; 121K
Wanajulikana sana na ugumu wao haswa pale wakiwa uwanjani kwao Turf Moor, hawana muda mrefu sana toka kupanda ligi kuu lakini bado haina makali katika mtandao huu.

16. West Bromwich Albion (16)
Wafuasi; 164K
Hawa majamaa wamefananisha msimamo wao katika ligi kuu na msimamo wao katika timu yenye wafuasi wengi kwa timu za ligi kuu, kote inashika namba 16.

15. Afc Bournemouth (17)
Wafuasi; 169K
Haina maisha mazuri katika ligi kuu, ikishika nafasi ya 17, nafasi moja tu juu ya mstali mwekundu wa kushuka daraja ila hawapo vibaya sana linapokuja swala la mtandao wa Instagram.

14. Watford (9)
Wafuasi; 172K
Imejitahidi kuwa na msimu mzuri ambapo kuna wiki kadhaa ilikaa kwenye nafasi 6 za juu katika msimamo wa ligi kuu. Lakini katika msimamo wa wafuasi wa Instagram inashika nafasi ya 14.

13. Swansea City (19)
Wafuasi; 203K
Bado inajikongoja na kujitahidi kurudi katika ufalme wao ule uliowafanya kubatizwa jina la Swanselona wakifananishwa na klabu ya Barcelona kipindi icho ikiwa chini ya kocha Brendan Rodgers. Inashika nafasi ya 13 kwa wafuasi wa Insta lakini nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi kuu.

12. Crystal Palace (20)
Wafuasi; 220K
Baada ya kuwa klabu ya kwanza kumtimua kocha wake Kelvin De Boer kutokana na kuanza vibaya na sasa ipo na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson klabu hiyo inajikongoja kwenye msimamo wa ligi kuu ila ipo vizuri Instagram.

11. Stoke city (14)
Wafuasi; 283K
Wapo chini ya kocha Mark Hughes na ikimilikiwa na kampuni ya kubetisha ya Bet365 inashika nafasi ya 11.

10. Southampton (13)
Wafuasi; 312K
Ipo chini ya mmiliki mfanyabiashara mwanamke ikipatikana katika uwanja wa Saint Mary ni klabu inayotisha na kuogopesha wengi kutokana na kikosi chake imara.

9. West Ham united (18)
Wafuasi; 472K
Ipo kwenye kizaazaa ambapo imetoka kumtimua kocha wake Slaven Bilic ambaye hajafanya vizuri na timu hiyo akiwaweka pabovu mwa msimamo wa ligi kuu licha ya kufanya usajili mkubwa.
Javier Hernandez, Arnautovic, Pablo Zabaleta na Joe Hart ni baadhi ya wachezaji waliovutwa na klabu hiyo lakini bado haijawa na msimu mzuri. Lakini sasa nafasi ya Bilic imechukuliwa na David Moyes.

8. Everton (15)
Wafuasi; 508K
Kati ya klabu zilizofanya usajili wa kukufuru na kufikia hatua kujaribu kuzaniwa Everton itafanya makubwa kwa usajili huo lakini imekuwa ndivyo sivyo. Ronald Koeman mwisho wa siku kutupiwa virago na klabu hiyo yenye makazi ya jiji la Liverpool.

7. Tottenham (3)
Wafuasi; 1.5M
Bado haina mizizi katika zao la wafuasi wengi wa soka katika mitandao. Kwa ukubwa na ukuu inayoionyesha klabu hiyo ingetegemewa klabu hiyo kuwa juu katika wafuasi na mashabiki wa soka.

6. Leicester (12)
Wafuasi; 1.8M
Unaweza ukashangazwa na hawa jamaa, lakini ndo hivyo, hawana muda mrefu sana katika ligi kuu toka wapande daraja lakini wapo vizuri kuliko hata hao wakongwe kwenye mtandao huo.
5. Liverpool (5)
Wafuasi; 5M
Majogoo wa jiji na wao wapo vizuri katika mtandao huo, huku kukiwa kuna kupanda na kushuka kwa klabu hiyo katika ligi kuu.

4. Manchester city (1)
Wafuasi; 5.6M
Ikiwa chini ya kocha Pep Guardiola, klabu ya Manchester city bado inajikongoja kujitanua na kutafuta mashabiki wengi huku pesa za mwarabu Sheikh Mansour akizidi kumwaga mapesa klabuni hapo.

3. Arsenal (6)
Wafuasi; 10.3M
Watoto wa Arsene Wenger na wajukuu wa Highbury stadium wanashika nafasi ya tatu katika wafuasi wengi katika ligi kuu.

2. Chelsea (4)
Wafuasi; 10.4M
Ukubwa wao katika ligi kuu sio mkubwa sana, lakini ilitambulika sana pale tu tajiri wa kirusi alipoinunua klabu hiyo.
Ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza ambapo msimu uliopita ilibeba taji hilo ikiwa na rekodi kibao.

1. Manchester utd (2)
Wafuasi; 19.6
Ni klabu tajiri duniani kwa sasa, lakini pia inaelezwa kwamba ndio klabu yenye mashabiki wengi duniani. Ukuu wao ulianzia pale Sir. Alex Ferguson alipoipa klabu hiyo mataji makubwa na klabu hiyo kujitangaza zaidi duniani.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.