Mshambuliaji mkali wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amekanusha vikali maneno na tuhuma ambazo watu na mashabiki wa soka wamekuwa wakimsakama.
Kumekuwa na tuhuma ambazo amekuwa akishambuliwa mchezaji huyo aliyeivusha timu yake ya taifa kucheza fainali za mwaka 2018 huko Urusi.
"kumekuwa na maneno yakisema huwa nachagua wachezaji ambao ni marafiki zangu kuchaguliwa timu ya taifa na makocha wa kuifundisha Argentina, nataka kukanusha na kukataa vikali kwamba hiyo sio kweli mimi nipo kwenye timu kama mchezaji wa kawaida tu" alisema Lionel Messi akiwa anahojiwa na chombo kimoja cha habari kipindi hiki akiwa na kikosi cha timu ya taifa kucheza michezo ya kimataifa.
Kumekuwa na tuhuma juu yake kwamba amekuwa akitumia ukubwa wa jina lake kuchagua nani na nani wanatakiwa kucheza timu ya taifa au hata kuifundisha.
Huku wengi wakisema anawachagua marafiki zake ambao anapatana nao akishinikiza waingie kwenye timu ya taifa.
"kusema Angel Di Maria, Javier Mascherano na Kun Aguero kwamba wao wanaingia timu ya taifa kwa vile nimewachagua kisa nipo nao karibu ni kuwakosea heshima wao na uwezo wao uwanjani" alimalizia Messi akiongea huku akionyesha amekasirishwa na tuhuma hizo.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.