Kumekuwa na fununu au tetesi ikielezwa klabu ya Real Madrid ipo katika mipango ya kumrudisha winga na mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr. katika ligi kuu ya Hispania ambapo winga huyo alitokea alipokuwa Barcelona.
Rais wa Real Madrid, Frorentino Perez inasemekana yupo katika mazungumzo na baba mzazi wa Neymar ambaye ni kama wakala wa nyota huyo ili kumsajili mchezaji huyo ambapo Madrid wenyewe wanasaka mtu wa kuweza kumrithi nyota Cristiano Ronaldo anayeonekana kupungua kiwango huku na umri ukizidi kumtupa mkono.
PSG ilimsajili Neymar akitokea Barcelona ya ligi kuu Hispania inapotokea pia klabu ya Real Madrid.
Neymar ndiye mchezaji ghali kwa sasa akiwa amesajiliwa kwa dau kubwa zaidi lililovunja rekodi ya dunia la paundi milioni 198.
Post a Comment
Post a Comment