Kama nilivyokwambia kuhusu michezo ya leo juu ya ugumu wake haswa ule mchezo wa Sevilla dhidi ya Liverpool ambapo matokeo yamewashangaza wengi mara baada ya Sevilla kutoka nyuma kwa mabao 3-0 mpaka kusawazisha na matokeo kuwa 3-3. Huku Spartak Moscow akitoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Maribor. Na msimamo wa kundi lao kuwa Liverpool bado akiongoza kundi akiwa na alama 9 huku Sevilla akifata akiwa na alama 8 na Spartak akiwa na alama 6.
Wakati hayo yakitokea kwa Sevilla na Liverpool, nako huko Ronaldo aiongoza Real Madrid kushinda 6-0 dhidi ya Apoel Nicosia, Ronaldo akifunga mara mbili.
Harry Kane na Heung Min Son wakaitoa Spurs nyuma ambapo ilifungwa 1-0 na Borrusia Dortmund na kufanya matokeo kuwa 2-1. Na kumfanya Tottenham kumaliza akiwa kileleni mwa kundi akifuzu kucheza hatua ya 16 bora, akifuzu pamoja na Real Madrid.
Napoli nao wakaigaragaza klabu ya Shakter Donetsk kwa kipigo cha magoli 3-0, magoli yakifungwa na Mertens, Insgne na Zielliski. Ambapo kwa matokeo haya Napoli ana nafasi ya kufuzu endapo Shakter atafungwa kwenye mchezo wa mwisho na Napoli ikishinda au ikitoa sare katika mchezo wa mwisho.
Lakini tatizo kubwa lipo kwa As Monaco ambao wanaonekana kupoteza makali yao mara baada ya kipigo cha mabao 4-1 mbele ya RB Leipzig huku mshambuliaji kinda wa klabu ya RB Leipzig, Werner akitupia mawili.
Matokeo mengine ni haya hapa chini;
Post a Comment
Post a Comment