Nyota wa klabu ya Manchester united, Anthony Martial anatakiwa na klabu ya Real Madrid ambayo ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 80 ili kumnasa nyota huyo raia wa Ufaransa.
Martial ambaye amekuwa hana uhakika wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza anatakiwa na klabu hiyo ambayo imekuwa na msimu mgumu kwa kipindi hiki, dau hilo linatajwa kupelekwa kwa klabu hiyo katika dirisha kubwa la usajili katika kipindi cha kiangazi.
Post a Comment
Post a Comment