Klabu tajiri duniani kwa sasa Real Madrid na Man utd zinaweza zikaingia kwenye vita nyengine, ukiachana na vita ya kugombania mashabiki.
Real Madrid imepanga kuishtukiza Man utd juu ya kuwa na mpango wa kutaka kumsajili nyota wa timu ambayo ni matajiri wa jiji la Manchester.
Madrid imepanga kupeleka maombi ya kumsajili Juan Mata ambaye ni raia wa nchini Hispania ambaye kwa sasa anaonekana kutokuwa na nafasi katika kikosi hicho huku akionekana kutokuwa katika mipango ya kocha Jose Mourinho ambaye alishawai kumuuza pindi kocha huyo na mchezaji huyo wakiwa klabuni Chelsea.
Kutokujumuishwa kwa mchezaji huyo katika kikosi cha Man utd kilichopokea kichapo dhidi ya Chelsea kunaelezwa ni kama nyota huyo hana maisha marefu klabuni hapo.
Post a Comment
Post a Comment