Mshambuliaji wa Barcelona ambaye ni raia wa Uruguay ya barani Amerika Kusini, Luis Suarez bado anaamini Phillipe Coutinho atajiunga na klabu ya Barcelona.

Suarez ambaye alishawai kucheza na Coutinho pindi wakiwa wote Liverpool ambapo Coutinho bado anaendelea kukichafua klabuni hapo anaamini licha ya Coutinho kushindwa kujiunga na klabu ya Barca katika dirisha la usajili lililopita lakini bado ataweza kujiunga na klabu hiyo katika dirisha dogo la majira ya baridi la mwezi januari kwa maana anaamini bado nyota huyo anatamani kuwa ndani ya Barcelona.

Coutinho ambaye ni raia wa Brazil ya barani Amerika Kusini alitajwa kwa karibu kujiunga na Barca ingawa klabu yake ya Liverpool ilipangua madili ambayo klabu hiyo iliyaleta kumsajili nyota huyo.

"Bado anatamani kujiunga na Barcelona, nachoamini ipo siku atakuja" alisema Suarez.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.