Ni Watford dhidi ya West Ham ingawa wengi watakuwa wanaangalia mchezo huu kama Watford dhidi ya David Moyes, kocha mpya wa West Ham aliyechukua nafasi ya Slaven Bilic kutokana na kuwa na matokeo mabovu.
Sasa macho yote kwa David Moyes, kila mtu anataka kuona atafanya nini katika nafasi hiyo mara baada ya kuwa na kariba mbaya toka alipotoka Everton na kuchaguliwa kuwa kocha wa Man utd na baadae kutimkia Real Sociedad ambapo kote huko akiwa na misimu mibovu.
Leo Moyes anaangaliwa yeye katika mchezo dhidi ya Watford ambapo atasafiri kwenda kwa Watford, je atafanikiwa kurudisha matumaini ya mashabiki wa West Ham waliochoshwa na matokeo mabovu? je atarudisha ubora wake ule aliokuwa nao pindi akiwa Everton?
Mchezo utaanza saa moja usiku.
Post a Comment
Post a Comment