Yani kwa sasa kilichobaki huko ligi kuu Hispania ni kuomba dua tu ili Barcelona apoteze, maana kwa moto alionao sasa si wa kawaida mara baada ya jana kuifunga Leganes magoli 3-0 huku Barcelona akiwa ugenini.
Luis Suarez baada ya ukame wa muda mrefu kwa kutokufunga lakini jana akasafisha nyota kwa kufunga mara mbili na jengine kufungwa na Paulinho, raia wa Brazil.
Lakini hii imekuwa ni zaidi ya maumivu kwa mashabiki wa klabu pinzani ya Real Madrid mara baada ya kusuluhu katika mchezo wa jana dhidi ya Atletico Madrid, matokeo yanayoifanya klabu hiyo kuachwa na Barca kwa alama 10.
Huenda labda kama Real Madrid watataka kulitetea taji lake la ligi kuu nchini Hispania walilolibeba msimu uliopita basi inabidi ipige maombi iiombee watani wake wakipoteza michezo zaidi ya mitatu ili wao warudi kileleni.
Ukame wa magoli wa Cristiano Ronaldo unazidi kumtesa yeye pamoja na klabu ambapo jana pia hakuonyesha kiwango kizuri, huenda hii tukaiita ni kuporomoka kwa ufalme wa Ronaldo? wote tunasubiri kuona cha muhimu bado ana mechi za kudhihirisha ubora wake kama mchezaji bora wa dunia zaidi ya mara tatu.
Post a Comment
Post a Comment