Kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Frank Lampard ametoa neno kuhusu fununu zinazomuhusu juu ya kuchukua nafasi iliyoachwa na Michael Emenalo.
Frank Lampard alikaririwa na gazeti moja la michezo akisema "Michael (Emenalo) ni mtu mzuri sana, nimefanya nae kazi nikiwa Chelsea kwa muda kama wa miaka 3 au 4, anahitaji kuthaminiwa na kupongezwa kwa kuifikisha timu ilipo ."
Michael Emenalo aliandika barua ya kuomba kujiuzulu katika nafasi yake ya uongozi klabuni hapo alipokuwa na cheo kinachomfanya ahusike zaidi na usajili wa wachezaji, akiwa amefanya kazi katika kiti hicho kwa miaka 10.
"Mi ni mtu wa Chelsea, na napenda kuendelea kuwa katika klabu hiyo kwa muda zaidi. Nikiipata nafasi hiyo itakuwa ni jambo la furaha kwangu" aliongezea Lampard ambaye aliisaidia Chelsea kutwaa mataji kadhaa akiwa kama mchezaji lakini pia ndiye mfungaji bora wa muda wote klabuni hapo.
Post a Comment
Post a Comment