Kombe la Dunia 2018 lipo mlangoni.
Ndicho unachoweza kukisema, mara baada ya kukamilika kwa kuwania kufuzu kwa timu zitakazoshiriki michuano hiyo lakini sasa kinachoangaliwa ni kupangwa kwa makundi ya kombe hilo ambapo kutakuwa na timu 32 na makundi 8 yatazigawa timu hizo ambapo kila kundi litakuwa na timu 4.
Gary Lineker ambaye ni mchezaji wa zamani wa Uingereza na Maria Komandnaya ambaye ni mwandishi wa habari za michezo nchini Urusi ndio wamechaguliwa kusimamia shughuli ya upangaji makundi hayo ambapo yatafanyika Urusi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Moscow tarehe 1 mwezi desemba.
Post a Comment
Post a Comment