Kocha wa West Bromwich, Tony Pulis ametupiwa virago na klabu yake hiyo mara baada ya mfululizo wa matokeo mabovu aliyoyapata.
Pulis alishuhudia klabu yake hiyo ikipoteza ikiwa nyumbani mbele ya Chelsea jumamosi iliyopita kwa mabao 4-0. Lakini pia katika michezo 6 iliyopita ya ligi kuu ameishia kupata sare 2 na kufungwa 4.
Gary Megson ambaye alikuwa kocha msaidizi amechaguliwa kuiongoza klabu hiyo mpaka pale itakapopata kocha mwengine.
Post a Comment
Post a Comment